
Agnes Mwandembo:
Ambonisye Mwandembo: |
Ambonisye Mwandembo:
MAISHA YA JAMII YA KIKRISTO
SEHEMU YA NNE
7. IBADA YA JAMII.
i). Ibada ya jamii ni ushirika na Mungu
Ibada ya jamii ni ushirika na Mungu. Huu ni wakati maalumu sana kwa jamii. Jamii ni ya thamani sana mbele zake Mungu. Mungu alifanya jamii. Aliazimu baba na mama na watoto waishi pamoja. Alitaka wafarijiane, na kusaidiana na kufundishana. Mungu anataka awepo katikati ya jamii yako. Anataka kuwa kichwa au kiongozi wa jamii yako. Anataka kuisaidia jamii yako ijue la kutenda au kufanya katika kila tatizo. Anataka wamsifu na kumshukuru.
Sehemu mbili za ibada ya jamii:- - Kumsikiliza Mungu - Kunena na Mungu
Ibada ya jamii ni tofauti na ibada ya kanisani. Katika kanisa muda wa ibada ni mrefu, wakati ibada ya jamii muda ni mfupi tu. Watoto wadogo na watoto wakubwa huabudu pamoja na wazazi wao.
- Kumsikiliza Mungu, huwa katika kunasoma Biblia. Tunapaswa tusichukue muda mrefu sana. Dakika tano, kumi tu inategemeana, kusoma na kutafakari neno. - Kunena na Mungu, huwa tunaimba, tunampa Mungu sifa. Na kuomba.
ii.) Ibada ya jamii ni kwa ajili ya jamii yote.
Mambo ya muhimu kujua kuhusu ibada ya jamii:- - Jamii inapaswa kuwa na ibada kila siku - Ni kwa ajili ya watu wote - Watu wote wanapaswa kushiriki na kufanya mambo yahusuyo.
Wakati mwingine inawezekana wakashindwa kufanya ibada ya pamoja, lakini wanapawa kufanya mpango huu kuona wanaweza kuabudu pamoja kila siku. Kuwa na jamii pamoja ni baraka kubwa. Kunafanya maisha yetu yawe ya furaha zaidi. Hii ni kazi kubwa na vilevile ina baraka. Kuwalea jamii zetu kwa ajili ya Mungu si rahisi inapasa kujitoa na kuvunja mipango mingine.
Baba na mama wanapata nafasi ya kuongoza na kufundisha jamii kwa njia hii ya ibada ya jamii kila siku. Jamii nyingine wanamwabudu Mungu asubuhi kabla ya kazi au shule. Wengine hufanya ibada jioni wakiisharudi nyumbani na baada ya shughuli zingine.
Unapaswa kuona muda mzuri ambao jamii yote inaweza kuhudhuria bila usumbufu wowote. Ni vizuri kuona wote nyumbani wanahudhuria hata pia wageni waliowatembelea. Kila mtu anaweza kufanya jambo fulani katika ibada hiyo kulingana na umri wake.
iii). Njia ya kuwa na ibada ya jamii.
Tunahitaji kutumia njia mbalimbali ili ibada iwe ya kupendeza siku zote. Tunapaswa tusisome na kuimba na kuomba kwa njia moja sikuzote. Kufanya hivi kila siku kunawachosha jamii.
Njia mbili mojawapo tunazoweza kuwa na ibada na jamii:- - Kujibu haja za jamii - Maswali na majibu - Kujifunza wimbo mpya - Kujifunza kwa moyo vifungu vya Biblia (kukariri Neno).
Haja za jamii: Kwa mfano mambo yanayohusu:- - Kifo katika jamii (YH. 14:2,3 1THE. 4:13-18) - Mmoja anakwenda safari au amesafiri (ZAB. 121) - Ugomvi katika jamii (EFE. 4:29 – 5:2) - Haja ya kujua uwezo mkuu wa Mungu (MWA. 1) - Haja ya kujua msamaha (1YOH. 1:5-10) - Haja ya kumtumaini Yesu (MK. 4:35-41)
Chagua vifungu ambavyo vinajibu haja ya jamii. Soma vifungu hivyo. Ongea pamoja maana ya vifungu hivyo. Nena pamoja jinsi ya kutii vifungu hivyo. Ombeni pamoja.
Kujifunza wimbo mpya: - Chagua wimbo mpya ambao mtu mmoja katika jamii anaujua - Jifunze kuimba pamoja - Nena maana ya maneno yake - Imbeni wimbo huo tena - Ombeni pamoja.
Kujifunza kwa moyo vifungu/kukariri: - Chagua vifungu kadhaa km. ZAB. 100, 121, 1KOR. 13:1-8, YAK. 1:2-12) - Jifunze kifungu kimoja kwa siku - Nena maana ya kifungu hicho - Nena kuhusu namna ya kumtii Mungu katika kifungu hicho - Rudia vifungu hivyo mara nyingi - Ombeni pamoja.
8. KUMWONGOZA MTOTO WAKO KWENYE WOKOVU.
Sisi sote tunataka watoto wetu waokoke na wafike mbinguni. Yesu anasema, “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi, kama sivyo ningeliwaambia, maana naenda kuwaandalia makao.. ili nilipo mimi nanyi muwepo” (YH. 14:2,3). Tungelitamani tuwepo na watoto wetu pamoja naye Kristo milele.
Hivyo mambo matatu muhimu ambayo wazazi wanapaswa kukumbuka kuhusu watoto wao ili kupata wokovu ni:- - Kuwatia moyo watoto wampokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wao binafsi - Kuwafundisha Neno la Mungu kwa ukamilifu - Kwa kuwaombea wapate neema hii.
Lakini lazima kila mtoto afikie kukata shauri yeye mwenyewe basipo kulazimishwa. Ili aweze kumpenda Mungu kwa moyo wake wote na kumtumikia yeye katika imani ya kweli.
Mambo matano ambayo tunapaswa kuelezea kuhusu kuokoka ni:- - Eleza sababu inayotufanya kuokoka. (RUM. 1:6-18). Ya kuwa Mungu ni mtakatifu. Sisi ni wenye dhambi. Hivyo, tunamhitaji Mungu ili tusamehewe na kutakaswa ili tuwe watakatifu. (1PET. 1:15,16).
- Eleza mambo ambayo Mungu amefanya ili kutuokoa. (RUM. 5:8). Ya kuwa Mungu alitupenda hata tulipokuwa tungali wenye dhambi. Alimtuma Yesu mwanawe ili afe na kutuchukulia adhabu ya dhambi zetu. (YH. 3:16. ISA. 53:4-11).
- Eleza njia ya kupokea wokovu. (RUM. 10:9,10. MDO. 3:19). Kwa njia ya kutubu dhambi na kuamini kweli moyoni, unapata msamaha wa dhambi, unamruhusu Yesu kuingia maishani mwako na kukufanya kiumbe kipya na kukaa naye. (UFU. 3:20, 2KOR. 5:17, YH. 1:12).
- Elezea ya kuwa unaweza kuishi maisha kumpendeza Mungu wakati wote wa maisha yako na kujilinda na mwovu. (1YOH. 3:1,2, 1YOH. 5:18,19).
- Elezea maisha yenye matumaini ya ufufuo katika kumngoja Yesu Kristo kuja kuwachukua alio wake. (1THE. 4:13-17 YH. 11:25, UFU. 1:7).
Mungu akubarikie!
|